NA MWANDISHI DIRAMAKINI
UTABIRI wa Hali ya Hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3 usiku wa leo Machi 7, 2022 unaletwa na mchambuzi, Daniel Masunga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara, Lindi, Ruvuma, Mtwara, Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Iringa, Mbeya na Njombe inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Aidha, mikoa ya Morogoro, Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
TMA inaeleza kuwa, mikoa ya Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Dar es Salaam na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia inatarajiwa hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Mkoa wa Tanga, visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Upepo wa Pwani
Kwa mujibu wa TMA, upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini Mashariki kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini.
Pia hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi madogo hadi makubwa kiasi.Matarajio kwa siku ya Jumatano ya Machi 09, 2022 pia mabadiliko kidogo yanatarajiwa.