Utabiri wa hali ya hewa saa 24 zijazo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UTABIRI wa hali ya hewa kuanzia leo saa tatu usiku unaletwa kwenu na mchambuzi, Tabu Kwedilima kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA mikoa ya Njombe, Lindi, Ruvuma na Mtwara kuna matarajio ya mawingu, mvua na ngurumo na vipindi vifupi vya jua.

Aidha, mikoa ya Morogoro (Kusini),Rukwa, Songwe, Iringa na Mbeya kuna matarajio ya mvua na ngurumo na vipindi vya jua huku Tabora, Kagera, Geita, Kigoma na Katavi matarajio yakiwa ni ngurumo na jua.

Mikoa ya Dodoma na Singida kuna matarajio ya mvua nyepesi na vipindi vya jua. Visiwa vya Unguja na Pemba, Dar es Salaam, Tanga, Morogoro (Kaskazini), Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia kuna matarajio ya jua.

UPEPO WA PWANI

Kwa mujibu wa TMA,upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini Magharibi kwa Pwani ya Kusini.

HALI YA BAHARI

Pia kwa mujibu wa TMA mawimbi makubwa kiasi yanatarajiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news