UTABIRI wa Hali ya Hewa kuanzia saa tatu usiku wa leo Machi 12, 2022 unaletwa kwenu na mchambuzi Tabu Kwedilima kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Ruvuma na Njombe matarajio ni mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
Kagera, Geita, Morogoro (Kusini), Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Songwe, Mbeya na Iringa hali ni mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma na Singida hali ni mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Dar es Salaam, Tanga, Visiwa vya Unguja na Pemba, Morogoro (Kaskazini), Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Pwani (ikijumuisha na Visiwa vya Mafia), Mwanza, Shinyanga, Simiyu na Mara: Matarajio ni jua.
UPEPO WA PWANI
Unatarajiwa kuvuma kutoka Mashariki kwa kasi ya Km 30 kwa saa kwa pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa kasi ya km 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini.
HALI YA BAHARI: Mawimbi madogo hadi makubwa kiasi yanatarajiwa
WEATHER FORECAST FOR THE NEXT 24 HOURS STARTING AT 9.00 P.M. DATE: 12/03/2022.
Today's weather forecast as presented by Daniel Masunga from Tanzania Meteorological Authority (TMA)