UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 zijazo kuanzia leo saa tatu usiku Machi 13, 2022 unawasilishwa na mchambuzi, Bi.Tabu Kwedilima kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Ruvuma, Morogoro (Kusini), Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa, Njombe, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Shinyanga na Simiyu kuna matarajio ya mvua,ngurumo na jua katika maeneo machache.
Aidha, mikoa ya Lindi, Mtwara, Dodoma na Singida kuna matarajio ya mvua nyepesi na jua katika maeneo machache.
Kwa upande wa Visiwa vya Unguja na Pemba, Dar es Salaam, Tanga, Morogoro (Kaskazini), Arusha, Manyara, Kilimanjaro, Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia kuna matarajio ya jua.
UPEPO WA PWANI
Kwa mujibu wa TMA, upepo huo unatarajiwa kuvuma kutoka Mashariki kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini Mashariki kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini.
HALI YA BAHARI
Mawimbi madogo hadi makubwa kiasi yanatarajiwa katika bahari.
TANZANIA WEATHER FORECAST 13/03/2022
THUNDERSHOWERS ARE EXPECTED OVER MWANZA, SHINYANGA, SIMIYU, MARA, GEITA, KAGERA, TABORA, KIGOMA, KATAVI, RUKWA, MBEYA, SONGWE, MOROGORO(KUSINI), IRINGA, NJOMBE AND RUVUMA REGIONS.