*Angalizo la mvua kubwa limetolewa kwa baadhi ya maeneo ya Kigoma, Katavi, Tabora, Dodoma, Singida na Manyara, Machi 17, 2022
*Kuna uwezekano wa kutokea mvua za wastani au kiwango cha athari, athari zinazoweza kujitokeza ni baadhi ya makazi kujaa maji, kuathirika kwa shughuli za usafirishaji
NA MWANDISHI DIRAMAKINI
UTABIRI wa hali ya hewa kuanzia saa tatu usiku wa leo Machi 16,2022 unawasilishwa na mchambuzi Noel Mlay kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Ruvuma, Lindi, Mtwara, Arusha, Manyara, Dodoma, Singida, Morogoro (Kusini), Kigoma, Katavi, Tabora, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe kuna matarajio ya mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.
Kwa mujibu wa TMA, Kilimanjaro, Morogoro (Kaskazini), Mwanza, Mara, Kagera, Geita, Shinyanga na Simiyu kuna matarajio ya mawingu ya mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
Aidha, kwa upande wa Dar es Salaam na Pwani ikijumuisha visiwa vya Mafia kuna matarajio ya mvua katika maeneo machache na jua. Tanga pamoja na visiwa vya Unguja na Pemba kuna matarajio ya mvua nyepesi na jua.
UPEPO WA PWANI: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kaskazimi Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
HALI YA BAHARI: Mawimbi makubwa kiasi yanatarajiwa.
TANZANIA WEATHER FORECAST 16/03/2022
ADVISORY HEAVY PRECIPITATION AT TIMES ARE EXPECTED OVER SOME AREAS OF KIGOMA, KATAVI, TABORA, SINGIDA, DODOMA AND MANYARA REGIONS.