*MAWINGU, MVUA NA NGURUMO VINATARAJIWA KWA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA RUKWA, MBEYA, SONGWE, IRINGA, NJOMBE, TABORA, SINGIDA, DODOMA NA RUVUMA
NA MWANDISHI DIRAMAKINI
UTABIRI wa hali ya hewa kuanzia saa tatu usiku leo Machi 17,2022 unaletwa na mchambuzi Noel Mlay kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Mikoa ya Ruvuma, Tabora, Dodoma, Singida, Morogoro (Kusini), Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe kuna matarajio ya mawingu, mvua na vipindi vya vifupi vya jua.
Lindi, Mtwara, Kigoma, Katavi, Morogoro (Kaskazini), Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Mwanza, Mara, Kagera, Geita, Shinyanga na Simiyu kuna matarajio ya mvua na ngurumo katika maeneo machache na jua.
Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ikijumuisha na visiwa vya Mafia kuna matarajio ya mvua nyepesi katika maeneo machache na jua. Huku Tanga na Visiwa vya Unguja na Pemba kuna matarajio ya jua.
UPEPO WA PWANI: Unatarajiwa kuvuma kutoka Kaskazini Mashariki kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani ya Kusini.
HALI YA BAHARI: Mawimbi madogo hadi makubwa kiasi.
WEATHER FORECAST 17/03/2022
CLOUD AND THUNDERSHOWERS ARE EXPECTED OVER SOME AREAS OF RUKWA, MBEYA, SONGWE, IRINGA, NJOMBE, TABORA, SINGIDA, DODOMA AND RUVUMA REGIONS.