*MVUA NA NGURUMO INATARAJIWA KATIKA MAENEO MENGI YA NCHI
NA MWANDISHI DIRAMAKINI
UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 kuanzia saa tatu usiku leo Machi 21, 2022 unaletwa na mchambuzi Noel Mlay kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, Kisiwa cha Unguja, Dar es Salaam, Morogoro (Kusini) Lindi, Mtwara, Ruvuma, Kigoma, Katavi, Tabora, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Kagera, Mwanza, Geita, Shinyanga, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe kuna matarajio ya mvua na ngurumo kwa maeneo machache na jua.
Aidha, mikoa ya Mara na Simiyu kuna matarajio ya ngurumo na jua huku Morogoro (Kaskazini) kuna matarajio ya mvua na vipindi vya jua.
Mikoa ya Tanga, kisiwa cha Pemba, Dodoma, Singida, Kilimanjaro, Arusha na Manyara kuna matarajio ya mvua nyepesi na jua.
UPEPO WA BAHARI: Unatarajiwa kuvuma kutoka Kusini Mashariki kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani yote.
HALI YA BAHARI: Kuna matarajio ya mawimbi makubwa kiasi.
WEATHER FORECAST 21/03/2022:
THUNDERSHOWERS IS EXPECTED OVER MANY AREAS OF THE COUNTRY.