*MVUA NA NGURUMO INATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA TABORA,
KIGOMA, KATAVI, KAGERA, GEITA, MWANZA, SHINYANGA, SIMIYU NA MARA
NA MWANDISHI DIRAMAKINI
UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 zijazo, kuanzia saa 3 usiku wa leo Machi 27,2022 unawasilishwa na mchambuzi Daniel Masunga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Mikoa ya Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu na Shinyanga inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Visiwa vya Unguja na Pemba, mikoa ya Iringa, Lindi, Mtwara, Ruvuma, Kilimanjaro, Manyara, Arusha, Tanga, Morogoro, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Mikoa ya Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kutoka Kusini Mashariki kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani yote.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi madogo huku matarajio kwa siku ya Jumanne tarehe 29 Machi,2022 huenda kukawa na mabadiliko kidogo.
TANZANIA WEATHER FORECAST 27/03/2022:THUNDERSHOWERS IS EXPECTED OVER SOME AREAS OF TABORA, KIGOMA, KATAVI, KAGERA, GEITA, MWANZA, SHINYANGA, SIMIYU AND MARA REGIONSWeather forecast for the next 24 hours starting tonight at 9:00 p.m on 27.03.2022 as presented by weather analyst, Daniel Masunga from Tanzania Meteorological Authority (TMA).