Utabiri wa hali ya hewa Tanzania saa 24 zijazo/Weather forecast March 28th,2022 starting 21:00 tonight

*MVUA NA NGURUMO ZINATARAJIWA KATIKA MAENEO MACHACHE YA MIKOA YA LINDI NA MTWARA

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

UTABIRI wa hali ya hewa kwa siku ya leo Machi 28,2022 kuanzia saa 9:00 usiku unaletwa na mchambuzi Daniel Masunga kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), Lindi na Mtwara kuna matarajio ya mawingu, mvua,ngurumo na vipindi vifupi vya jua.

Visiwa vya Pemba na Unguja, Dar es Salaam, Tanga, Morogoro, Pwani (ikijumuisha visiwa vya Mafia), Kigoma, Tabora, Katavi, Kilimanjaro, Manyara, Arusha, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe, Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu na Shinyanga inatarajiwa kuwa na mvua, ngurumo na jua.

Pia mikoa ya Ruvuma na Iringa inatarajia mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua huku Dodoma na Singida ikitarajiwa kuwa na mvua nyepesi na jua.

UPEPO WA PWANI: Unatarajiwa kuvuma kutoka Kusini Mashariki kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani yote.

HALI YA BAHARI:Mawimbi madogo.

WEATHER FORECAST 28/03/2022: CLOUD, THUNDERSHOWERS ARE EXPECTED OVER FEW AREAS OF LINDI AND MTWARA REGIONS
  Weather forecast for the next 24 hours as presented by Magreth Massawe from Tanzania Meteorological Authority (TMA).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news