*MVUA ZINATARAJIWA KUONGEZEKA ZAIDI KUSINI NA MAGHARIBI MWA TANZANIA HII INASABABISHWA NA UWEPO WA UKANDA WA MVUA MAENEO HAYO
NA MWANDISHI DIRAMAKINI
UTABIRI wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3 usiku,leo Machi 30,2022 unaowasilishwa na mchambuzi Godfrey Kazinja kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Kigoma, Tabora, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Iringa na Njombe inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vifupi vya jua.
Visiwa vya Unguja na Pemba, Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Mara, Simiyu, Shinyanga, Kilimanjaro, Manyara, Arusha, Tanga, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Mikoa ya Dodoma na Singida inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kutoka Kusini Mashariki kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kwa Pwani yote.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo huku matarajio kwa siku ya Ijumaa ya Aprili Mosi, 2022 yakitarajiwa mabadiliko kidogo.
TANZANIA WEATHER FORECAST 30/03/2022:CLOUD, THUNDERSHOWERS ARE EXPECTED OVER FEW AREAS
Weather forecast for the next 24 hours starting tonight at 9:00 p.m on 30.03.2022 as presented by weather analyst Godfrey Kazinja from Tanzania Meteorological Authority (TMA).