NA GODFREY NNKO
YUAN ya China inanunuliwa kwa shilingi 361.153 huku ikiuzwa kwa shilingi 364.620 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.6 na kuuzwa kwa shilingi 19.77.
Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 152.521 na kuuzwa kwa shilingi 153.9 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.04 na kuuzwa kwa shilingi 20.21.
Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2287 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.9.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Machi 14, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 2998.9 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3029.86 na Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2519.36 na kuuzwa kwa shilingi 2545.48.
Wakati huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.24 na kuuzwa kwa shilingi 2.29 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania