NA GODFREY NNKO
LEO Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 151.2 na kuuzwa kwa shilingi 152.65 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.0002 na kuuzwa kwa shilingi 20.165.
Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2287.02 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.9.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Machi 16, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 2988.91 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3019.03 na Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2513.9 na kuuzwa kwa shilingi 2539.95.
Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 358.56 huku ikiuzwa kwa shilingi 362.1 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.41 na kuuzwa kwa shilingi 19.59.
Wakati huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.24 na kuuzwa kwa shilingi 2.29 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania