NA GODFREY NNKO
LEO Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.4 huku ikiuzwa kwa shilingi 362.94 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.94 na kuuzwa kwa shilingi 19.12.
Aidha,Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 153.92 na kuuzwa kwa shilingi 155.43 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 19.983 na kuuzwa kwa shilingi 20.15.
Dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1698.6 na kuuzwa kwa shilingi 1716.03 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.06 na kuuzwa kwa shilingi 50.50.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Machi 23, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2287.04 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.9.
Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3022.8 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3053.9 na Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2514.83 na kuuzwa kwa shilingi 2540.90.
Wakati huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.23 na kuuzwa kwa shilingi 2.29 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64.
Kwa mujibu wa Benki Kuu, Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.7 na kuuzwa kwa shilingi 628.8 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) ikununuliwa kwa shilingi 146.76 na kuuzwa kwa shilingi 148.06.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania