*Pula ya Botswana inanunuliwa kwa shilingi 198.1 huku ikiuzwa kwa shilingi 200.7
NA GODFREY NNKO
LEO Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 155.13 na kuuzwa kwa shilingi 156.64 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 19.9 na kuuzwa kwa shilingi 20.13.
Dola ya Australia (AUD) inanunuliwa kwa shilingi 1712.56 na kuuzwa kwa shilingi 1729.91 huku Franka ya Ubeligiji (BEF) ikinunuliwa kwa shilingi 50.1 na kuuzwa kwa shilingi 50.50.
Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 359.20 huku ikiuzwa kwa shilingi 362.34 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 18.81 na kuuzwa kwa shilingi 18.99.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Machi 25, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2287.07 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.94.
Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3018.70 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3049.81 na Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2513.5 na kuuzwa kwa shilingi 2539.3.
Wakati huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.214 na kuuzwa kwa shilingi 2.258 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64.
Kwa mujibu wa Benki Kuu, Dirham (AED) ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) inanunuliwa kwa shilingi 622.7 na kuuzwa kwa shilingi 628.8 huku sarafu ya Austria ya Schilling (ATS) ikununuliwa kwa shilingi 146.8 na kuuzwa kwa shilingi 148.1.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania