NA GODFREY NNKO
LEO Franka ya Burundi inanunuliwa kwa shilingi 2.19 na kuuzwa kwa shilingi 2.21 huku dola ya Marekani nchini ikinunuliwa kwa Shilingi 2286.9604 na kuuzwa kwa Shilingi 2309.83.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa ya viwango elekezi vya kubadilisha fedha za kigeni iliyotolewa leo Machi 8, 2022 na Benki Kuu ya Tanzania (BoT).
Aidha,kwa mujibu wa BoT, Paundi ya Uingereza inanunuliwa kwa Shilingi 3018.102 huku ikiuzwa kwa Shilingi 3049.21 na Euro ya Ulaya inanunuliwa kwa shilingi 2488.442 na kuuzwa kwa shilingi 2514.25.
Yuan ya China inanunuliwa kwa shilingi 361.975 huku ikiuzwa kwa shilingi 365.5 na Yen ya Japan inanunuliwa kwa shilingi 19.85 na kuuzwa kwa shilingi 20.05.
Wakati huo huo, Franka ya Rwanda inanunuliwa kwa shilingi 2.21 na kuuzwa kwa shilingi 2.26 huku shilingi ya Uganda ikinunuliwa kwa shilingi 0.61 na kuuzwa kwa shilingi 0.64.
Kwa upande wa Randi ya Afrika Kusini inanunuliwa kwa shilingi 149.1003 na kuuzwa kwa shilingi 150.44 huku shilingi ya Kenya ikinunuliwa kwa shilingi 20.07 na kuuzwa kwa shilingi 20.23.
Tags
Bank of Tanzania Exchange Rates
Benki Kuu ya Tanzania
BoT
Fedha na Uchumi
Habari
Indicative Exchange Rates from Bank of Tanzania