Wanawake NSSF warejesha tabasamu kwa wagonjwa waliolazwa Hospitali ya Rufaa Shinyanga

*Washukuru kwa kupatiwa mahitaji mbalimbali

NA KADAMA MALUNDE

WANAWAKE wanaofanya kazi katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga wamesherehekea Siku ya Wanawake Duniani kwa kutoa mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akikabidhi mahitaji mbalimbali kwa ajili ya wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani. (Picha zote na Malunde 1 blog).
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi akizungumza wakati Wanawake wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga wakikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani leo Machi 11,2022. 
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (wa nne kulia) akizungumza wakati Wanawake wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga wakikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (kushoto) akizungumza wakati Wanawake wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga wakikabidhi mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kukabidhi mahitaji hayo leo Machi 11,2022 katika wodi za wanawake na watoto, Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi amesema wamefika katika hospitali hiyo ili kutoa faraja kwa wanawake na watoto ikiwa ni sehemu ya kusherehekea siku ya Wanawake Duniani ambayo husherehekewa ulimwenguni kote Machi 8.

“Sisi wanawake kutoka NSSF Shinyanga tumekuja hapa kusherehekea siku ya wanawake duniani na wanawake ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga kwa kuleta mahitaji mbalimbali ikiwemo sabuni za unga na miche, mafuta ya kujipaka,pipi,biskuti, maji na juisi,”amesema Mdabi.
Sehemu ya mahitaji mbalimbali ikiwemo sabuni za unga na miche, mafuta ya kujipaka,pipi,biskuti, maji na juisi vilivyotolewa na Wanawake wafanyakazi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akikabidhi sabuni ya unga na mahitaji mengine kwa Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (wa nne kulia) kwa ajili ya wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake Duniani.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akikabidhi sabuni ya unga na mahitaji mengine kwa Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (wa nne kulia) kwa ajili ya kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani.
Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy (katikati) akiangalia mahitaji mbalimbali yaliyotolewa na Wanawake wanaofanya katika Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) Mkoa wa Shinyanga kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.
Wauguzi na wanawake wafanyakazi NSSF Shinyanga wakijiandaa kugawa mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani.
Wauguzi na wanawake wafanyakazi NSSF Shinyanga wakijiandaa kugawa mahitaji mbalimbali kwa wanawake na watoto waliolazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kusherehekea Siku ya Wanawake duniani.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi akikabidhi mafuta ya kujipaka kwa mmoja wa wanawake wodini. Kila mwanamke wodini amepatiwa mafuta,sabuni ya unga na mche,juisi, pipi na maji.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi akikabidhi mafuta ya kujipaka kwa mmoja wa wanawake wodini. Kila mwanamke wodini amepatiwa mafuta,sabuni ya unga na mche,juisi, pipi na maji.
Wanawake NSSF Mkoa wa Shinyanga wakimwangalia mtoto aliyelazwa wodini wakati wakikabidhi mahitaji mbalimbali.
Afisa Uandikishaji Mwandamizi NSSF Mkoa wa Shinyanga, Rose Robert akikabidhi sabuni na mafuta kwa mmoja wa wanawake wodini.
Afisa Mkuu Mwandamizi wa NSSF Mkoa wa Shinyanga, Amina Mdabi (kushoto) akizungumza na mama anayeuguza mtoto wake wodini.
Wanawake wafanyakazi NSSF Mkoa wa Shinyanga wakiwa wodini.
Zoezi la kukabidhi mahitaji mbalimbali wodini likiendelea.
Zoezi la kukabidhi mahitaji mbalimbali wodini likiendelea.

Naye Muuguzi Wodi 3 A katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga, Victoria Mmasy akizungumza kwa niaba ya Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo amewashukuru wanawake hao kwa kufika katika hospitalini hapo na kutoa mahitaji kwa akina mama na watoto waliolazwa.

Nao akina mama waliolazwa katika hospitali hiyo wamewashukuru wanawake hao kutoka NSSF mkoa wa Shinyanga kwa kuwapatia mahitaji hayo ambayo yatawasaidia katika kipindi hiki wakiendelea kupatiwa huduma za matibabu hospitalini hapo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news