Watumishi wanawake taasisi za elimu ya juu lindeni watoto wenu-Tume

NA MWANDISHI MAALUM

KATIBU Msaidizi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma, Bw. Salvatory Kaiza amewaasa watumishi wanawake kutoka katika taasisi za umma na binafsi za elimu ya juu kukemea na kufichua vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia kwa watoto wa kike.

Ameyasema hayo Machi 3,2022 katika mafunzo ya nidhamu na utaratibu wa undeshaji wa mashauri ya nidhamu sehemu za kazi yaliyoandaliwa na Chama cha Wafanyakazi wa Taasisi za Elimu ya Juu (THTU)- wanawake Taifa katika Ukumbi wa maktaba ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii Kijitonyama, Dar es salaam.
Wafanyakazi wa taasisi za umma na binafsi za elimu ya juu wakipata mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyofanyika katika Ukumbi wa maktaba ya Taasisi cha Ustawi wa Jamii.
Wafanyakazi wa taasisi za umma na binafsi za elimu ya juu wakipata mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyofanyika katika ukumbi wa maktaba ya Taasisi cha Ustawi wa Jamii.
Bw. Salvatory Kaiza akizungumza na wafanyakazi wa taasisi za umma na binafsi wakati wa mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyofanyika Machi 3,2022 katika ukumbi wa maktaba ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii,Kijitonyama Dar es salaam.

"Nidhamu ni suala la muhimu sana kwa watumishi wa umma ili kufikia malengo ya taasisi, ni vyema wafanyakazi kuzingatia sheria, taratibu na kanuni mahali pa kazi ili kufanikisha utendaji wa kazi katika taasisi,kulinda utumishi wetu na tumalize utumishi wetu salama pia kuwalinda watoto wetu hasa wa kike waliopo vyuoni,” amesema Kaiza.

Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt. Eventus Mugyabuso amepongeza mafunzo hayo huku akisisitiza kuwa, mwanamke ndiye mhanga mkuu pale mtumishi wa umma yeyote anapoadhibiwa akifanya makosa iwe yeye mwenyewe au iwe familia, hivyo ni jambo jema sana kwa mafunzo hayo kuandaliwa na wanawake wa THTU Taifa ambaye Mwenyekiti wake ni mhadhiri msaidizi kutoka katika taasisi yao ya Ustawi wa Jamii.
Kaimu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Dkt. Eventus Mugyabuso akizungumza na wafanyakazi wa taasisi za elimu ya juu (hawapo pichani) waliohudhuria mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi. Mafunzo yaliyoandaliwa na watumishi wanawake wa Chama cha Watumishi wa Elimu ya Juu na kufanyika katika ukumbi wa maktaba ya Taasisi ya Ustawi wa Jamii, Kijitonyama Dar es salaam.

Kwa upande wake Prof. Sotco Claudius Komba ambaye ni Makamu Mkuu wa Taasisi Taaluma, aliwakaribisha wafanyakazi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii na watumishi wanawake wa taasisi za elimu ya juu waliofika kushiriki katika mafunzo hayo ambayo yatasaidia katika ustawi wa nidhamu kazini na amewashukuru wote kwa kuja kupata mafunzo hayo.
Makamu Mkuu wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii taaluma, Prof. Sotco Claudius Komba akizungumza na wafanyakazi wa taasisi za umma na binafsi wakati wa wafunzo ya nidhamu mahali pa kazi yaliyoandaliwa na watumishi wanawake wa taasisi za elimu ya juu wa Chama cha Watumishi wa Taasisi za Elimu ya Juu.

“Nawakaribisha sana katika Taasisi ya Ustawi wa Jamii na tunashukuru kwa kuja kuendesha mafunzo haya kwenye taasisi yetu, tunaamini mafunzo haya yatatupa mwangaza kuhusiana na nidhamu kwa wafanyakazi,”amesema Prof.Komba.
Bw. Salvatory Kaiza, Katibu Msaidizi Tume ya Utumishi wa Umma (kushoto) akifuatiwa na Bi Salma Fundi Mwenyekiti Jumuiya ya Wanawake THTU Taifa na Mwenyekiti wa THTU Taifa, Dkt.Paul Loisulie.

Kaimu Mratibu Msaidizi kamati ya wanawake THTU, Bi. Roselyne Mathew Massam amesema, mafunzo hayo yameratibiwa na Chama cha Wanawake THTU kuelekea kwenye Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani yenye lengo la kusaidia watumishi kuelewa umuhimu wa nidhamu mahali pa kazi, kupunguza migogoro kazini na ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi.

Aidha, Bi. Roselyne Massam ameomba Tume ya Utumishi wa Umma kuongeza wafanyakazi wanaoshughulikia mashauri ya nidhamu sehemu za kazi ili kuongeza kasi ya utendaji na kupunguza ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi.
Dkt.Paul Loisulie ambaye ni Mwenyekiti wa THTU Taifa akichangia mada wakati wa mafunzo ya masuala ya nidhamu mahali pa kazi yaliyoandaliwa na watumishi wanawake wa Chama cha Watumishi wa Taasisi ya Elimu ya Juu na kufanyika katita Ukumbi wa Taasisi ya Ustawi wa Jamii.

“Tunaomba tume iongeze watendaji ili kusaidia kuongeza kasi ya utendaji na kupunguza ucheleweshwaji wa rufaa kwa mfanyakazi,mashauri mengi yanachukua muda mrefu na inachukua muda mrefu kwa mfanyakazi kurudishwa kazini,” amesema Bi. Roselyne.

Mafunzo hayo ya siku moja yaliandaliwa na wanawake wa THTU kuelekea kilele cha Siku wa Wanamke Duniani tarehe 8 Machi,2022.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news