Waziri Aweso: Acheni visingizio vya kuunganisha maji kwa wateja

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

WAZIRI wa Maji, Juma Aweso amezitaka mamlaka za maji kuacha visingizio kuunganishia maji wateja isizidi wiki moja.
Aweso aliyasema hayo kwenye Kijiji cha Msoga Halmashauri ya Chalinze wilayani Bagamoyo baada ya ziara ya Kamati ya Bunge ya Maji, Kilimo na Mifugo ilipotembelea kuona miradi ya maji maeneo ya Mlandizi, Chamakweza na Msoga.

Amesema kuwa, kwa kuwa wananchi wana ari ya kupata huduma ya maji hawataki kusikia mtu anakaa miezi sita bila ya kuunganishiwa maji zisizidi siku saba kwani wanafanya jitihada hawataki kusikia eti viungo havipo.

Aidha, amezitaka mamlaka hizo kujadiliana na wadaiwa sugu namna gani watakavyolipa madeni yao na baada ya makubaliano wawarejeshee huduma ya maji kwa wale waliowakatia.

Naye Mwenyekiti wa kamati hiyo, Dkt.Christine Ishengoma amesema kuwa, mambo yanakwenda vizuri jinsi mamlaka wanavyogawa maji yanakwenda hadi Morogoro kupitia mitambo ya Ruvu Juu na Ruvu Chini watu wa Morogoro na Pwani na Dar es Salaam watakuwa na huduma za uhakika.

Naye Mtendaji Mkuu wa DAWASA, Cyprian Luhemeja alisema kuwa kwa mradi wa Chamakweza utaenda hadi Morogoro ambapo hiyo ni hatua ya kwanza na ya pili itakuwa ni kusambaza kwa wananchi.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge alisema kuwa kwa sasa kuna mradi mkubwa kutoka Bwawa la Mwalimu Nyerere Rufiji utakaotoa lita milioni 7.5 kwa siku pia Bwawa la Kidunda nalo litatia maji mengi hivyo Pwani na Dar es Salaam maji yatapatikana ya kutosha na taasisi zote za serikali zimeunganisha vipaumbele vya mkoa kwani kuna mkakati wa pamoja baina ya wizara hizi kupitia kamati na watahakikisha maji yanawafikia wale wa chini.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news