Waziri Aweso achukua hatua kwa Mamlaka ya Maji Karatu, asema timu ya wataalamu itawasili huko

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

SERIKALI imesema itatuma timu ya wataalamu wa Sekta ya Maji kuangalia uhalisia wa gharama za huduma ya maji zinazotozwa kwa wateja mbalimbali mjini Karatu mkoani Arusha.
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amesema hayo Februari 28,2022 baada ya kufanya ziara maalumu ya kikazi mjini Karatu na kupokea taarifa ya utoaji wa huduma ya maji katika mji huo.

Waziri Aweso, amepokea taarifa hiyo katika kikao na wadau wa sekta ya maji mjini Karatu ambapo bei ya maji imebainika kuwa kubwa na upangaji wake kukosa vielelezo muhimu.

Kufuatia sintofahamu hiyo, Waziri Aweso ameivunja Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Karatu (KARUWASA). Mji wa Karatu unahudumiwa na Jumuiya ya KAVIWASU na KARUWASA.

Waziri Aweso ameahidi wakazi wa Karatu kuwa, Serikali itafanya mabadiliko makubwa katika utoaji wa huduma ya maji kufuatia ukaguzi alioufanya katika ofisi za KARUWASA, na kusisitiza kutekeleza mageuzi makubwa ya utendaji katika mamlaka hiyo.

Ameongeza kuwa, kiasi cha shilingi bilioni nne zitaelekezwa mjini Karatu ili kuboresha miundombinu ya maji katika kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji kwa bei rafiki.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news