*Asisitiza anataka kuona wanachukua hatua mapema kabla mambo hayajaharibika katika halmashauri
NA MWANDISHI MAALUM, OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe.Innocent Bashungwa amewataka Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wote nchini kuhakikisha wanashughulikia changamoto za halmashauri mapema kuliko kusubiria mpaka tume ziunde kwenda kuchunguza.

"Ninyi ni wasimamizi wa halmashauri kwenye mikoa yenu, ikiwa mambo hayaendi sawa katika eneo lolote ni rahisi kujua mapema, sasa kwa nini msidhibiti changamoto hizo mnasubiria mpaka TAMISEMI tulete tume wakati uwezo na mamlaka mnayo? Alihoji Mhe. Bashungwa na kuongeza kuwa,
"Sasa nataka kuona mnachukua hatua mapema kabla mambo hayajaharibika huko, hii itasaidia kupunguza malalamiko na shughuli za maendeleo kutekelezwa kwa ubora".

Mhe. Bashungwa alihitimisha kikao hicho kwa kuwataka viongozi hao kuendelea kuongeza usimamizi kwenye Ukusanyaji wa Mapato ya ndani ya Halmashauri ili kufikia Malengo ya kukusanya zaidi ya shilingi Trilioni moja kwa mwaka wa fedha wa 2022/23.