NA MWANDISHI MAALUM
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe, Mohamed Mchengerwa amewataka watendaji wote wa wizara yake kujitafakari utendaji wao na kufanya kazi kwa kuzingatia weledi ili kuendelea kuleta mapinduzi makubwa kwenye Sekta ya Utamaduni, Sanaa na Michezo.

"Naomba niwatake watendaji wote kufanya kazi kwa kufuata maadili na taratibu za kazi za Serikali ili kuleta mafanikio kwa wananchi kwa ujumla,"amefafanua Mhe. Mchengerwa.
Amewataka Wakuu wa Idara wote kuwa na vikao vya kiutendaji na watumishi wao ili kuleta mageuzi ya kiutendaji na kuwataka watendaji kufanya kazi kama timu moja huku wakifungua milango ya wadau kama wasanii ili kujua haki zao.
“Watendaji tokeni waelezeni wasanii ili waweze kujisajili ili waweze kupata haki zao na wapate manufaa,”amesema.
Kwa upande mwingine, Mhe. Mchengerwa amesema Wizara imefanya mambo makubwa kwenye sekta za michezo, sanaa na Utamaduni na kwamba kinachotakiwa sasa ni kuendelea kufanya vizuri.
