Waziri Mchengerwa: Serengeti Girls (U17) mnalipa heshima kubwa Taifa, hongereni

*Asema timu hiyo inastahili pongezi nyingi

NA JOHN MAPEPELE

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe.Mohamed Mchengerwa ameipongeza Timu ya Taifa U-17 Serengeti Girls kwa kuishinda timu ya Taifa ya Botswana mabao 4-0 katika mchezo wa kufuzu kucheza kombe la Dunia 2022 nchini India.

Mhe. Mchengerwa amesema timu ya Serengeti Girls inastahili pongezi kwa kuwa imeendelea kuiheshimisha Tanzania katika mashindano ya Kimataifa.
"Nilipoitembelea kambini wiki iliyopita huko Zanzibar nilifanya vitu viwili,niliwapa jina rasmi la Serengeti Girls na niliwapa mikakati, ninafurahi kuona wamelitendea haki jina hilo na mikakati tuliyowapa wameitekeleza,"ameeleza Mhe. Mchengerwa.

Timu ya Taifa ya Wanawake U17 ya Serengeti Girls imeweza kufuzu mzunguko unaofuata baada ya kuwatoa Botswana kwa jumla ya magoli 11 kwa 0 baada mechi ya awali iliyopigwa Zanzibar kushinda 7-0 na jana marudiano kushinda magoli 4-0 yaliyofungwa na Neema Paul 1 na Clara Luvanga 3.

Baada ya mchezo huu mchezo unaofuata Serengeti Girls watapambana na Timu ya Taifa ya Burundi.

Mashindano ya Dunia ya Soka la Wanawake chini ya miaka 17 yanafanyika Oktoba 2022 India baada ya kupata wawakilishi wa FIFA toka kila bara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news