Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipokea kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella orodha ya majina ya awali ya kaya 86 zenye watu 453 ambao wamekubali kuondoka kwenye Hifadhi ya Ngorongoro kwa hiari yao huku wengine wakiendelea kujiandikisha, wakati akizungumza na viongozi wa kimila wa Wamasai 'Laigwanan' kwenye eneo maalum la mikutano la Marya ambalo ni sehemu ya kufanyia ibada za mila na bunge linalojadili na kutatua migogoro ya Jamii ya Wamasai lililopo kwenye viwanja vya Chuo cha Ufundi Arusha, Machi 10, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na viongozi wa kimila wa Wamasai ‘Laigwanan’ wakati alipowasili katika eneo maalum la mikutano la Marya ambalo ni sehemu ya kufanyia ibada za mila na bunge linalojadili na kutatua migogoro ya Jamii ya Wamasai lililopo kwenye viwanja vya Chuo cha Ufundi Arusha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifanyiwa maombi maalum na viongozi wa kimila wa Wamasai ‘Laigwanan’ wakati alipozungumza nao kwenye eneo maalum la mikutano la Marya ambalo ni sehemu ya kufanyia ibada za mila na bunge linalojadili na kutatua migogoro ya Jamii ya Wamasai lililopo kwenye viwanja vya Chuo cha Ufundi Arusha.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akivishwa vazi la heshima na viongozi wa kimila wa Wamasai wakati alipozungumza nao kwenye eneo maalum la mikutano la Marya ambalo ni sehemu ya kufanyia ibada za mila na bunge alinalojadili na kutatua migogoro ya Jamii ya Wamasai lililopo kwenye viwanja vya Chuo cha Ufundi Arusha, Machi 10, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na viongozi wa kimila wa Wamasai ‘Laigwanan’ kwenye eneo maalum la mikutano la Marya ambalo ni sehemu ya kufanyia ibada za mila na bunge linalojadili na kutatua migogoro ya Jamii ya Wamasai lililopo kwenye viwanja vya Chuo cha Ufundi Arusha, Machi 10, 2022. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).