Waziri Prof.Mbarawa atoa maagizo kwa TRC kuhusu reli ya kisasa

NA MWANDISHI MAALUM

WAZIRI wa Ujenzi na Uchukuzi Prof. Makame Mbarawa amewataka Viongozi wa Shirika la Reli Nchini (TRC) kuhakikisha ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro kilomita 300 unakamilika na kuanza majaribio ya awali mwishoni mwa mwezi Aprili.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), Prof. John Kondoro akimuonesha Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa sehemu ya kupangia mabehewa ya Reli ya Kisasa ya SGR katika eneo la Kwala mkoani Pwani. (Picha na WUU).

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi huo Prof. Mbarawa amesema muda wa ujenzi wa sehemu ya kwanza Dar es Saalam hadi Morogoro sasa ufike mwisho ili watanzania waanze kunufaika na matunda ya uwekezaji mkubwa uliofanywa na Serikali kwa ajili yao.

“Ifikapo mwisho wa mwezi ujao nataka kazi ya ujenzi wa sehemu hii iwe imekamilika na treni ya majaribio ianze kazi,”amesisitiza Prof. Mbarawa.
Muonekano wa majengo ya karakana ya Reli ya Kisasa ya SGR katika eneo la yakiwa hatua za mwisho za ujenzi wake Mkoani Pwani. (Picha na WUU).

Aidha, amezungumzia umuhimu wa kuweka mifumo ya kisasa ya kielekroniki katika kukata tiketi na kupata wapangaji watakaotoa huduma bora na za kisasa katika stesheni zote za reli hiyo.

Ameitaka TRC kuandaa mpango wa kutunza miundombinu yake yote ya reli, treni na majengo ili kuiwezesha kudumu kama ilivyokusudiwa. Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa akitandika na kukaza Reli ya Kisasa ya SGR, katika eneo la Kwala, Mkoani Pwani.(Picha na WUU).

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika hilo Prof. John Kondoro amesema ujenzi wa reli hiyo umefikia asilimia 95 na asilimia 5 zilizobaki zitakamilika katika muda mfupi ujao.

Amemhakikishia Waziri Prof. Mbarawa kuwa mikakati ya kuiwezesha reli ya kisasa nchini iko katika hatua nzuri na maelekezo yote yaliyotolewa yatazingatiwa.
Muonekano wa karakana ya Reli ya Kisasa ya SGR, katika eneo la Kwala, Mkoani Pwani. (Picha na WUU).

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TRC Bw. Masanja Kadogosa amesema tayari shirika limeingia Mkataba wa kununua mabehewa 1430 yatakayotumika katika reli hiyo.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Reli Tanzania (TRC), Prof. John Kondoro (kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo. Bw. Masanja Kadogosa wakimsikiliza Mtaalam wa Biashara na Miliki wa TRC (kulia), walipokagua jengo la abiria katika stesheni Kuu ya Reli ya Kisasa ya SGR jijini Dar es Salaam. (Picha na WUU).

Aidha, amesema tayari wafanyakazi 600 wako katika hatua za mwisho za kuajiriwa ili kuhakikisha huduma zitakapoanza ziwe za uhakika kama ilivyokusudiwa.

Kukamilika kwa reli ya SGR licha ya kuwa kutaboresha huduma za usafiri na uchukuzi nchini pia kutapunguza ajali za barabarani zinazosababishwa na msnogamano wa magari na kupunguza uchafuzi wa mazingira kwa kupunguza uzalishaji wa kaboni kwa kuwa reli hiyo itakuwa ikitumia umeme na hiyo kuifanya Tanzania kuwa moja ya nchi zinazotumia usafiri wa reli wa viwango vya juu.
Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa, akisisitiza jambo kwa Mwenyekiti wa Bodi ya TRC, Prof. John Kondoro na wataalam wa Mkandarasi Yapi Markez, alipokagua maendeleo ya ujenzi wa SGR, Mkoani Pwani. (Picha na WUU).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news