Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha sita ambao mwaka huu watafanya mitihani yao ya mwaka, wakiwa bado na uzuni juu ya kuteketea kwa moto vifaa vyao vilivyokuwemo ndani ya bweni la wanawake skuli ya Utaani, wakati wa kikao na Waziri wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar huko Wete.
Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Mohamed Nassor Salim akitoa taarifa ya janga la moto lililotokea katika bweni la wanawake skuli ya Utaani Wete, kwa mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, walimu na wananchi.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohamed Mussa akizungumza katika hafla ya kuwafariji wanafunzi ambao walipata mtihani wa bweni lao kuungua moto hivi karibuni, huko katika skuli ya utaani Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Pemba, Salama Mbarouk Khatib akizungumza katika kikao cha kuwafariji wanafunzi waliopata mtihani wabweni lao kuungua moto hivi karibuni, katika kikao cha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Harusi Said Suleiman akizungumza na wanafunzi, walimu na wazazi wa wanafunzi waliopata na mtihani wa bweni lao kuungua moto la skuli ya utaani hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Ifraj Zanzibar Foundation, Abdalla Said Abdalla akizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 20, kwa uongozi wa Skuli ya Utaani kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha sita ambao wanatarajia kufanya mitihani yao ya taifa, ambapo vifaa vyao viliteketea kwa moto.
Mwakilishi wa Bodi ya Milele Zanzibar Foundation, Ali Bakar Hamad akizugumza katika hafla ya kukabidhi vifaa vyenye thamani ya shilingi Milioni 20, kwa wanafunzi wa kidato cha tano hadi cha kwanza kwa skuli ya sekondari Utaani, ambao bweni lao lilipata mtihani wa kuungua moto hivi karibuni.
Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Pemba, Mfamau Lali Mfamau akizungumza katika hafla ya kuwafariji wanafunzi ambao bweni lao lilipata mtihani wa kuungua moto hivi karibuni.
Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Pemba, Mohamed Nassor Salim akijadiliana jambo na watendaji kutoka Wizara hiyo wakati wa kikao cha Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohamed Mussa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Harusi Said Suleiman, walipofika kuwafariji wanafunzi wa Skuli wa Utaali waliopata mtihani wabweni lao kuungua moto hivi karibuni. (Picha na Abdi Suleiman).