Zanzibar yadhamiria kukabiliana na maradhi ya figo

NA RAHIMA MOHAMED-Maelezo

KATIBU Mkuu Wizara ya Afya Zanzibar, Dkt.Fatma Mrisho amesema hospitali za kisasa zinazojengwa katika maeneo mbalimbali nchini zitakuwa na vitengo maalum vya kusafisha damu kwa wagonjwa wa maradhi ya figo.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Dkt. Fatma Mrisho akisisitiza jambo wakati akitoa hotuba ya Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani yaliofanyika katika Uwanja wa Hospitali Mnazi Mmoja Zanzibar.

Akizungumza katika Siku ya Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani kwa niaba ya Waziri wa Afya amesema ugonjwa wa figo ni hatari sana, hivyo kuwepo kwa kitengo hicho kutasaidia kuondoa usumbufu wa wagonjwa kufuata huduma katika Hospitali Kuu ya Mnazi Mmoja.

Aidha, amesema kuwepo kwa kitengo hicho kitasaidia kuimarisha afya za wagonjwa kwani wanapata usumbufu mkubwa wakati wanapohitaji matibabu.
Mkurugenzi Mtendaji Wizara ya Afya, Dkt. Marjani Msafiri akitoa hotuba ya makaribisho kwa mgeni rasmi katika Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani yaliofanyika katika Uwanja wa Hospitali Mnazi Mmoja Zanzibar..

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Mnazi Mmoja, Dkt.Msafiri Marijani amesema endapo wananchi watabadilisha mtindo wao wa maisha kwa kufuata maelekezo ya wataalam wa afya wanaweza kuepukana na maradhi tofauti.

Amesisitiza haja ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuweka miili sawa na kuepukana na maradhi nyemelezi.

Kuhusu tatizo la uhaba wa madaktari bingwa nchini, Dkt. Marijani amewashauri wataalam na wasomi wa kada ya Afya kusomea fani muhimu ikiwemo upasuaji mishipa ya damu, moyo, figo ili kupunguza idadi ya kupeleka wagonjwa nje ya Zanzibar kupata matibabu.
Msomaji risala, Dkt.Maryam Mohamed Hamad katika Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani yaliofanyika katika Uwanja wa Hospitali Mnazi Mmoja Zanzibar.

Akisoma risala daktari bingwa wa ugonjwa wa figo,Dkt.Mariam Hamad amesema wameandaa kampeni maalum ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari ikiwemo kutoa elimu kupitia vyombo vya habari,vipeperushi na mikutano ya wananchi katika shehia mbalimbali nchini.
Baadhi ya wageni waalikwa waliohudhuria katika maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani yaliofanyika katika Uwanja wa Hospitali Mnazi Mmoja Zanzibar.

Aidha, amesema kitengo chao kinakabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo uhaba wa wafanyakazi, chumba cha upasuaji kwa ajili ya kusafishia damu na uwekaji vifaa pamoja na mafundi wa mashine zinapoharibika.
.
Shuhuda wa maradhi ya figo, Balozi Ramadhan Muombwa akitoa nasaha kwa waliopata maradhi na madaktari katika Maadhimisho ya Siku ya Figo Duniani yaliofanyika katika Uwanja wa Hospitali Mnazi Mmoja Zanzibar.

Siku ya figo duniani huadhimishwa kila ifikapo tarehe 10 Machi ya kila mwaka ambapo kauli mbiu yake kwa mwaka huu ni “afya ya figo kwa wote”.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news