NA MWANDISHI WETU
MKUU wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi amesema kuwa, Abdulrahman Kinana ambaye jina lake limependelezwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni mtu mwenye uwezo mkubwa na kuwataka kuachana na mambo ya nyuma.

"Hakuna ubishi juu ya uwezo wa Mzee Kinana," ameeleza Hapi huku akifafanua kuwa Kinana ni mtu mwenye uwezo, maarifa na uzoefu mkubwa kwenye siasa na ni mwalimu kwa watu wengi kwenye chama hicho.
"Kama vijana ambao tunaendelea kujifunza kwenye siasa za chama mambo ya nyuma nadhani hayana msingi kwa sasa hivi,"amesema.