NA DIRAMAKINI
MIGODI ya Barrick ya North Mara na Bulyanhulu imetoa msaada wa vipimo vya kisasa vya utambuzi wa magonjwa katika hospitali mbili za mikoa kama sehemu ya mpango wa kusaidia nchi katika kupambana na kukabiliana na ugonjwa wa UVIKO-19 na magonjwa mengine ya kuambukiza.
Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara , Apolinary Lyambiko, akimkabidhi mashine za vipimo kwa viongozi wa Serikali wa Mkoa wa Mara.
Viongozi wa Chama na Serikali mkoani Mara katika picha ya pamoja na maofisa wa Barrick katika hafla hiyo.
Katika hafla ya kukabidhi msaada huo katika Hospitali ya Rufaa ya
Musoma, Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Apolinary Lyambiko,
alikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Ally Happi,
vifaa vya kisasa vya kupima magonjwa ya kuambukiza kama virusi vya
UVIKO-19, Kifua Kikuu, Nimonia, Mafua makali na magonjwa mengineyo.
Daktari
Mkazi katika mgodi wa North Mara, Dkt. Nicholas Mboya, alibainisha kuwa
utambuzi unaweza kufanywa kupitia aina mbalimbali za sampuli, kwa
kuchukua vipimo kwenye pua, Koo, mate au makohozi, na kutoa majibu kati
ya muda wa dakika 49 na 80.
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Ally Happi, akiongea katika hafla ya kupokea vifaa vya vipimo (Kushoto) ni Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara , Apolinary Lyambiko
Meneja Mkuu wa Mgodi wa North Mara, Apolinary Lyambiko, akiongea katika hafla ya kukabidhi mashine za kisasa za kupima magonjwa.
Mganga Mkuu wa Mkoa (RMO) wa Mara, Dkt Juma Mfanga akiongea wakati wa hafla hiyo.
Wageni waalikwa katika hafla hiyo wakifuatilia matukio.
Alisema,upimaji huu unadhihirisha ubora wa vipimo hivi vya kisasa ambavyo vinaweza kutambua majibu ya sampuli nne kwa wakati mmoja.
"Tunajivunia kutoa vifaa hivi maalum ili kuimarisha miundombinu ya matibabu katika jamii zinazozunguka migodi ya kampuni," Lyambiko alisema.