DC Kiteto awasilisha maombi maalumu kwa RC Makongoro Nyerere

NA MOHAMED HAMAD

MKUU wa Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Mbaraka Al Haji Batenga amewasilisha maombi maalumu kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Charles Makongoro Nyerere ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika mji wa Kibaya na uwekaji wa taa, ukarabati wa barabara ya kuunganisha Kata ya Engusero na Orkine ya kiwango cha Changarawe pamoja na ujenzi wa daraja la Kuunganisha Kata ya Kibaya na Bwagamoyo.

Maombo hayo yanagharimu shilingi Bilioni 1.72, ambapo kama yatafanikiwa wananchi wa maeneo hayo wataondokana na adha ya wagonjwa kusafirishwa kwa magari kwenda hospitali hata wakulima kushindwa kufikisha mazao yao wanapotoka shambani.
"Mheshimiwa Mkuu wa mkoa, wilaya tumeona tukukabidhi maombi yetu haya ya fedha, ili uyawasilishe Serikalini na kwa wadau wengine wa maendeleo tukiamini unayo nafasi ya kukutana nao na kuwasilisha kilio chetu hiki ili wananchi waweze kuondokana na adha hii,"amesema Mkuu wa Wilaya ya Kiteto.

Aidha, akizungumza baada ya kupokea maombi hayo Mkuu huyo wa Mkoa wa Manyara, Mhe.Charles Makongoro Nyerere amesema, hana budi kupokea maombi hayo kwani anajua wananchi wa Kiteto wana changamoto kubwa ya barabara.

"Ni kweli kwa ujumla na hata wakati tukipata maelekezo kutoka kwa Mheshimiwa Rais pamoja na mambo mengine tulitakiwa kushughulikia migogoro ya ardhi na alitaka pia tusimamie kikamilifu fedha za ujenzi wa barabara kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA),"amesema.

Amesema, kwa mamlaka aliyonayo atapaza kilio hicho ambacho anaamini kama fedha hizo zitapatikana zitakuwa msaada mkubwa kwa wananchi wa maeneo tajwa ambayo wamekuwa wakipata adha kubwa kwa kukosa huduma hiyo.

Akizungumzia barabara hizo, Patrick Shila ambaye ni Mwenyekiti wa Kitongoji cha Majengo Kaloleni alisema kuanzishwa kwa TARURA nchini kumefungua barabara nyingi ambapo wengi wa wananchi wa eneo lake walishindwa kufikisha mazao yao sokoni yanapotoka shambani kwa kukosa barabara.

"Tunaomba Serikali kupitia TARURA waendelee kufungua barabara zaidi, kwani bado kuna changamoto ambazo zinahitaji jitihada za maksudi kuendelea kuzifungua ili wananchi waweze kufika katika maeneo yao kwa urahisi,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news