Dkt.Mkamilo:TARI imedhamiria kufanya mambo makubwa kwa maslahi ya Taifa na manufaa kwa Watanzania

NA DIRAMAKINI

MKURUGENZI Mkuu wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania (TARI), Dkt. Geoffrey Mkamilo amesema, taasisi hiyo inaendelea kuwekeza kwa nguvu katika usambazaji wa teknolojia na kutumia vyombo vya habari kusambaza habari mbalimbali za tafiti za kilimo kwa manufaa ya Watanzania na maslahi mapana ya Taifa.
Dkt. Mkamilo ameyasema hayo leo katika kikao kazi cha viongozi Wakuu wa Idara na vituo 17 vya taasisi hiyo.

Dkt. Mkamilo amesema kuwa, taasisi imepata mafanikio ya usambazi wa teknolojia za kilimo kupitia vyombo vya habari.
Dkt. Mkamilo amewataka wakurugenzi na Mameneja wa Vituo kuweka umuhimu katika kuhakikisha kuwa Usambazaji wa Teknolojia kupitia njia mbalimbali za mawasiliano unasimamiwa kikamilifu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news