*RPC wa Dodoma, Onesmo Lyanga apelekwa Makao Makuu ya Polisi Dodoma
NA GODFREY NNKO
MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, IGP Simon Sirro amefanya uhamisho na mabadiliko ya baadhi ya Makamanda wa Polisi wa mikoa ambapo amemuhamisha RPC wa Dodoma, Onesmo Lyanga kwenda Makao Makuu ya Polisi Dodoma na nafasi yake imechukuliwa na aliyekuwa RPC Kaskazini Unguja, Martin Otieno.