NA DOREEN ALOYCE
JESHI la Uhamiaji Mkoa wa Dodoma linawashikilia raia watano wa Ethiopia akiwemo Mtanzania mmoja kutokana na kuingia nchini kinyume cha sheria na utaratibu wa nchi.
Pia linamshikilia raia mmoja wa Tanzania, Tito Mbwilo mwenye umri wa miaka 43 mkazi wa Iringa na Tunduma ambaye alikuwa akisafirisha wahamiaji hao.

"Jeshi letu la uhamiaji tumefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu watano akiwemo mtanzania mmoja wakisafirishwa kwenye gari yenye namba za usajili T991 DXB Toyota Rumion ambalo lilikuwa linaendeshwa na Tito Mbwilo akijua ni kosa,"alisema Bahati.

Hata hivyo, alitoa onyo kwa wasafirishaji wote wanaojihusisha na wahamiaji haramu katika Mkoa wa Dodoma kuacha mara moja na kwamba jeshi tayari limebaini wamebadili mbinu kutoka magari makubwa na kutumia magari madogo.
"Niwaombe wananchi wote wakiwemo wa Mtera kuendelea na ushirikiano kutoa taarifa za kusafirisha wahamiaji haramu jambo ambalo litasaidia katika utendaji kazi wetu,"alisema Bahati.