Each 7 April is Karume Day in Tanzania to remember the legacy of Abeid Karume, the first president of Zanzibar and the first Vice President of Tanzania.
NA DIRAMAKINI
RAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Alhaj Dkt. Hussein
Ali Mwinyi ameongoza hitma ya kumuombea dua Rais wa Kwanza wa Zanzibar,
marehemu Sheikh Abeid Amani Karume, iliyofanyika Ofisi Kuu ya CCM
Kisiwandui Zanzibar.
Hitma
hiyo, pia ilihudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Samia Suluhu Hassan pamoja na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo
Rais Mstaafu wa Zanzibar wa Awamu ya Sita, Dkt. Amani Abeid Karume,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango.
Wengine
ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Kassim Majaliwa,
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Othman Masoud Othman, Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, viongozi wa vyama vya
siasa pamoja na viongozi wa dini.
Hitma
hiyo ya kumuombea dua Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume ambapo pia ni
miongoni mwa maadhimisho ya Siku ya Mashujaa ilitanguliwa na dua ya
ufunguzi kutoka kwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa
Salum na Qur-an tukufu, iliyosomwa na Ustadh Abdulrahim Twalib na
kuhitimishwa na Sheikh Salim Juma Faki.
Mara
baada ya hitma hiyo, Sheikh Khamis Abdulrahman, Mjumbe wa Baraza la
Maulamaa Zanzibar alitoa mawaidha na kumuelezea marehemu mzee Abeid
Amani Karume kuwa ni kiongozi aliyepigania maendeleo ya wananchi wa
Zanzibar na kumuombea MwenyeziMungu ampe makaazi mema Peponi. Amin.
Aidha, Sheikh Khamis alieleza kwamba kumuombea dua mtu aliyetangulia mbele ya haki ni wajibu kwa kila Muislamu.
Aliongeza
kuwa miongoni mwa mambo mengi mazuri aliyoyafanya Marehemu Sheikh Abeid
Amani Karume pia, ameweka misingi mizuri ya taalum kwa kujenga na
kuweka jiwe la msingi la Chuo Cha Kiislamu kilichopo Mazizini Zanzibar
mnamo mwaka 1972, chuo ambacho kimetoa wataalamu pamoja na Maulamaa
mbali mbali ambao wengine hivi sasa wako ndani na nje ya Tanzania
wakitoa elimu waliyoipata chuoni hapo.
Aidha,
tukio lililofuata ni uwekaji wa mashada ya mauwa ambapo walioweka maua
katika kaburi la Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume ni Rais wa Zanzibar
na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Hussein Ali Mwinyi, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, Mkuu wa Majeshi
ya Ulinzi ya Tanzania Venance Salvatory Mabeyo kwa niaba ya wakuu wa
vikosi vya Ulinzi Tanzania.
Wengine
ni Balozi mdogo wa India anayefanya kazi zake hapa Zanzibar Bhagwant
Singh aliyewawakilisha Mabalozi wenzake wa hapa nchini, Balozi Ali
Karume aliyewakilisha familia ya Marehemu Sheikh Abeid Amani Karume
pamoja na Mzee Ramadhan Nzori aliyeweka shada la maua akiwawakilisha
wazee.
Pia,
katika tukio hilo kulisomwa dua na sala vilivyoongozwa na viongozi wa
dini katika kaburi la Marehemu Sheikh Abeid Karume lililopo pembezoni
mwa Afisi hiyo ya CCM Kisiwandui ambapo Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh
Omar Kabhi alisoma kwa niaba ya Waislamu, Padri Stanley Nikolas Lichinga
Katibu wa Dayosisi ya Anglikana Zanzibar alisoma kwa niaba ya Wakristo
pamoja na Nikhil Mahraja Joshi Kandka aliyesoma kwa niaba ya Wahindu.
Aidha,
wake wa viongozi wakiongozwa na Mama Mariam Mwinyi walihudhuria katika
hitma hiyo ambapo pia, Mjane wa Marehemu Sheikh Abeid Karume Mama Fatma
Karume na viongozi wengine wanawake wa kitaifa wakiwemo Mawaziri,
Wabunge, Wawakilishini pamoja na wake wa viongozi wastaafu na wananchi
kutoka sehemu mbali mbali za Zanzibar na Tanzania Bara.
April
7, 1972 ndiyo siku aliyouawa Rais wa Kwanza wa Zanzibar marehemu Mzee
Abeid Amani Karume na wapinga maendeleo nchini ambapo leo imetimia miaka
50 tokea utokee msiba huo.