NA OR-TAMISEMI
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhe. Innocent Bashungwa amewaagiza wakuu wa wilaya mkoani Kagera kusimamia kikamilifu maelekezo ya Serikali iliyoyatoa kwenye zao la kahawa na kuhakikisha bei wanayolipwa wakulima inakuwa sawa na bei ya soko katika msimu husika.
Mheshimiwa Bashungwa ametoa maelekezo hayo katika mkutano wa wadau wa maendeleo wilayani Karagwe mkoani Kagera wa kujadili ufungamanishaji wa kilimo na uchakataji malighafi viwandani uliofanyika Aprili 28, 2022.

Bashungwa amesema, Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa katika ziara yake wilayani Karagwe alitoa maelekezo kuondolewa kwa tozo 42 kati ya 47 ambazo walikuwa wanatozwa wakulima wa kahawa wa Mkoa wa Kagera.


Pia amemwagiza Mkurugenzi wa Bodi ya Kahawa na Mkurugenzi wa Maendeleo ya Mazao wa Wizara ya Kilimo na timu yake kukaa Mkoa wa Kagera katika msimu wote kusimamia maelekezo ya Serikali iliyoyatoa kwenye zao la kahawa.