Mamia ya watalii kutoka Israel wawasili Tanzania

NA DIRAMAKINI

BODI ya Utalii Tanzania (TTB) imeshiriki katika mapokezi ya watalii 780 kutoka nchi ya Israel ambao wamewasili nchini Tanzania siku ya Aprili 16, 2022 kwa lengo la kutembelea vivutio vya utalii. Watalii hawa wametumia ndege nne za kukodi ambazo zimefanya safari zake za moja kwa moja kutoka nchini ya Israel.
Watalii wakitoka katika ndege mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA).

Ujio wa watalii hawa ni matokeo ya kazi ya TTB ya kutangaza vivutio vya utalii kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Israel, Taasisi za Wizara ya Maliasili na Utaii pamoja na Mawakala wa utalii wa Tanzania kwa kushiriki Maonesho ya utalii yanayojulikana kama International Mediterranean Tourism Market (IMTM) yanayofanyika kila mwaka katika mji wa Tel Aviv nchini Israel.

Aidha,Aprili 9, Tanzania ilipokea kundi la watalii 267 na April 13, 2022 waliwasili watalii 165 hivyo mpaka sasa tumepokea jumla ya watalii 1, 212 kutoka Israel. Wakiwa hapa nchini, watatembelea vivutio vya utalii vya Hifadhi za Taifa za Arusha, Tarangire, Manyara, Ngorongoro, vikundi vya utalii wa kiutamaduni na visiwa vya Zanzibar.Watalii wakiwa wanapata huduma kiwanja cha ndege cha KIA. Wahudumu wa ndege wakipata picha ya kumbukumbu na wanakikundi ngona za kimasai cha KIA.

“Tanzania Imefunguka, ugeni ni huu ni uthibitisho kuwa Tanzania ni salama hivyo watalii wajipange kuja Tanzania kutembelea vivutio vya asili. TTB tunaendelea kushirikiana na wadau wa utalii bega kwa bega kuhakikisha kwamba tunapenye kwenye masoko mengine mapya ya utalii na kuwavutia watalii wengi zaidi.” 

Hayo aliyasema Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB, Jaji Thomas Mihayo wakati wa Mapokezi katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (KIA).

Jaji Mihayo aliwapongeza Mawakala wa utalii wa Tanzania kwa ushirikiano mzuri na Mawakala wa Israel kwa pamoja wameweza kufanikisha kuwashawishi wananchi wa Israel kuichagua Tanzania kuwa ”best destination” kwa mwaka 2022. Kwa juhudi hizi, Tanzania itaendelee kupokea makundi mengi zaidi ya Watalii kutoka nchi mbalimbali duniani. Watalii wakiwa wanaelekea katika lango la kutokea mara baada ya kuwasili.
Watalii wakifurahia mara baada ya kupata huduma katika kiwanja cha KIA

Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TTB ni miongomi ya watu waliohudhuria mapokezi hayo, wengine ni Mwakilishi kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA), Bi Catherine Mbena na Mwakilishi kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro, ndugu Peter Makutiani.

Takwimu za mwaka 2020 zinzonyesha Tanzania ilipokea watalii 6,880 kutoka nchi ya Israel.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news