Mchumi ataja sababu kuu tatu za mafuta kupanda bei kwa kasi duniani

NA GODFREY NNKO

AFISA Mkuu wa Fedha wa Jimbo la Connecticut nchini Marekani, Bw. Lunda Asmani ametaja sababu kuu tatu ambazo zimechangia bei za bidhaa hususani mafuta kupanda kwa kasi duniani.
Bw.Asmani ameyasema hayo wakati akielezea kuhusiana na namna ambavyo uvumilivu unahitajika katika kipindi hiki ambacho Dunia inakabiliana na changamoto za bidhaa mbalimbali kupanda bei kwa kasi.

"Kusema kweli, bei ya mafuta imepanda, na imeanza kupanda kwa kasi sana Duniani kote, lakini kuna sababu kuu tatu za kiuchumi ambazo zimechangia bei ya mafuta kupanda.

"Kwanza, itakumbukwa kuwa, kipindi kile cha UVIKO-19 imepamba moto, watu wengi mizunguko ilikuwa imepunguzwa sana, wafanyakazi walikuwa wanafanya kazi kutoka majumbani, usafiri wa anga, usafiri wa barabara ulikuwa umepungua sana, hivyo ule uhitaji wa mafuta ulikuwa umepungua, yaani ile demand (uhitaji) ya mafuta ilikuwa imeshuka sana,"amesema Bw.Asmani.

Amefafanua kuwa, kwa wastani wanasema, Marekani mtumiaji wa kawaida wa mafuta alikuwa amepunguza matumizi ya mafuta kwa karibu asilimia 50, kwa sababu ya kutozunguka na watu walikuwa wanafanya kazi nyumbani, na mizunguko ya safari ilikuwa imepungua kutokana na janga la UVIKO-19.

"Sasa unakuta katika hali hiyo, wakati uhitaji wa mafuta ulikuwa umpungua pia kiuchumi na bei ya mafuta huwa inashuka yaani 'supply and demand' kipindi hicho kutokana na uhitaji wa mafuta kuwa mdogo,"amesema.
Bw.Asmani amesema jambo la pili ambalo linalingana na hilo,ni kwamba kipindi hicho wakati uhitaji wa mafuta umepungua na uzalishaji pia, wazalishaji wa mafuta wenye walipunguza uzalishaji,kwa sababu uhitaji ulikuwa mdogo.

"Kwa hiyo kama wangeendelea na uzalishaji kabla wakati ule wa UVIKO-19, wangejikuta kwamba wana malighafi ambayo haina mnunuzi, kwa hiyo na wao walipunguza sana uzalishaji wa mafuta, kwa hiyo hali hiyo ikatengeneza hali ya uhaba.

"Kama mnavyofahamu katika uchumi, panapokuwa na uhaba wa kitu chochote kile, bei ya hiyo bidhaa huwa inapanda. Kwa hiyo kutokana na ule uhaba,wa uzalishaji wa mafuta kutokana na uhitaji wa mafuta kuwa mkubwa,na wenyewe sasa umeanza kuchangia kuongezeka kwa bei ya mafuta.

"Na sasa hivi, nchi zimeanza kufunguka,watu wameanza kurudi makazini, watu wameanza kusafiri na mipaka imeanza kufunguliwa, sasa unakuta ule uhitaji wa mafuta umepanda, lakini ule uzalishaji bado ulikuwa katika kile kiwango cha ule uhitaji mdogo,na bado haujafikia ule uhitaji wa sasa, sasa inapotokea katika hali hiyo,unakuta kwamba, bei ya bidhaa yoyote ile kama uhitaji ni mkubwa na uzalishaji ni mdogo itapanda bei na ndivyo ilivyo kwa bei ya mafuta,"amefafanua Bw.Asmani.

Wakati huo huo, Bw.Asmani ametaja jambo la tatu ambalo limechangia bei ya mafuta kupanda kwa kasi duniani kuwa inachochewa na vita kati ya Urusi na Ukraine.

"Jambo la tatu ni hii vita ya Urusi kuivamia nchi ya Ukraine, kwamba kutokana na vikwazo ambavyo mataifa ya Magharibi yameanza kuiwekea Urusi,kama mnavyofahamu nchi ya Urusi ni mzalishaji mkubwa wa mafuta, vile vikwazo sasa vinachangia katika kupunguza uzalishaji wa mafuta.

"Kwa sababu yale mafuta ambayo Urusi ilikuwa ikiyauza nchi za nje, nchi za nje sasa zimeacha kununua mafuta kutoka Urusi,hivyo sasa imepunguza soko, hivyo kama nilivyosema awali unapokuta soko limepungua na mahitaji yapo juu, basi bei zinakuwa zimepanda.

"Kwa hiyo kuna vitu vikuu vitatu ambavyo vimetokea kwa wakati mmoja,ambavyo vimechangia hili la bei ya mafuta kuwa juu na hii si kwa nchi moja tu, ni kwa nchi zote duniani, popote pale ulipo ukifungua gazeti au ukiangalia taarifa ya habari, taarifa nyingi za habari zinaanza na hilo la bei ya mafuta, kama kawaida bei ya bidhaa au mafuta huwa inapanda na kushuka, kwa hiyo tuna imani kwamba baada ya muda hili litasawazika na bei zitarudi kama kawaida, kama tulivyozoea wananchi,"amefafanua Bw.Asmani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

2 Comments

  1. The problem here is fear and greed. So far there no oil wells or pipelines damaged during Covid19 or Ukrainian Russia war. On the other hand, Ukrainian and Russia war is a brother to brother conflict, how come the whole world if affected. There is no evidence supply and demand shortages!!

    ReplyDelete
  2. The problem here is fear and greed. So far there no oil wells or pipelines damaged during Covid19 or Ukrainian Russia war. On the other hand, Ukrainian and Russia war is a brother to brother conflict, how come the whole world if affected. There is no evidence supply and demand shortages!!

    ReplyDelete
Previous Post Next Post

International news