NA DIRAMAKINI
NAIBU Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Bw.Ramadhan Kailima amelipongeza Jeshi la Uhamiaji nchini kwa kupata mafanikio makubwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Samia Suluhu Hassan.
Ameyasema hayo Aprili 4, 2022 katika Chuo cha Uhamiaji cha Kikanda (TRITA) kilichopo Moshi mkoani Kilimanjaro wakati akifungua Kikao cha Baraza la Wafanyakazi wa Jeshi la Uhamiaji nchini.