NA DIRAMAKINI
MOJA wapo ya changamoto katika kupambana na ukatili wa kijinsia na ukatili dhidi ya watoto ni kuchelewa kwa taarifa ambazo jamii inazifahamu.
Picha na Refuge.
Kutokana na changamoto hiyo, watumishi wa wizara za kisekta wameendelea kutoa mchango wao kwa kutoa namba za asimu ili jamii ipate wepesi wa kutoa taarifa.
Sambamba na kutumia namba ya Kitaifa ya 116 ya SEMA inayotoa huduma bila malipo saa 24 kila siku.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu tarehe 17,2022 namba zifutazo hapa chini zitatoa hamasa na kasi ya uwasilishaji wa taarifa za viashiria vya ukatili au za matukio ya ukatili.
Ikumbukwe kuwa, Serikali inatekeleza Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili kwa Wanawake na Watoto wa mwaka 2017/18 hadi 2022.
Aidha, Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum kwa ushirikiano na Wizara za Kisekta itaendelea kuhuisha na kuongeza namba za simu za wilaya, halmashauri hadi kata ili huduma iwe karibu zaidi na jamii. Zifuatazo hapa chini ni jina la muhusika, ofisi husika, namba ya simu na taarifa za ziada;