
Septemba 2, 2021 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati akisalimia wananchi wa eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam aliwaeleza Watanzania faida ya kipindi cha filamu maarufu cha Royal Tour chenye lengo la kuitangaza Tanzania katika angaza za Kimataifa kwenye eneo la vivutio vya utalii, maeneo ya uwekezaji, sanaa na utamaduni wa watu wa Tanzania, filamu ambayo ameigiza maeneo mbalimbali ya vivutio nchini Tanzania akiwa kama Mhusika Mkuu.