NA DIRAMAKINI
SERIKALI chini ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) iliweka kipaumbele utoaji wa elimu ya fedha kwa Watanzania hususani vijana kwa malengo ya kukuza jamii iliyo na uelewa na masuala ya fedha.

Elimu hiyo inaelekezwa katika ufunguaji wa akaunti za benki na utunzaji wa akiba kwa manufaa ya baadae.

Afisa wa benki ya NMB Idara ya Uwajibikaji kwa Jamii, Aloyce Kikois, aliwasisitiza wanafunzi juu ya uwekaji wa akiba na kutumia benki kama sehemu sahihi ya kuhifadhi fedha kwani ni salama zaidi.
Kwa mujibu wa Meneja wa Benki ya NMB Idara ya Uwajibikaji kwa Jamii, Lilian Kisamba alisema, Benki ya NMB tayari imetoa mafunzo hayo katika maeneo mbalimbali nchini huku zaidi ya watanzania 80,000 wakinufaika na elimu hii hasa katika ulimwengu wa sasa wa kiteknolojia.