*Tathimini ya utendaji kazi wa wakuu wa idara, vitengo na watumishi wengine katika mamlaka za Serikali za mitaa inaendelea ili kubaini ubora wa utendaji kazi wa watumishi hao
NA GODFREY NNKO
OFISI ya Rais-Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) imesema kuwa, inaendelea kufanya tathimini ya utendaji kazi wa wakuu wa idara, vitengo na watumishi wengine katika mamlaka za Serikali za mitaa ili kubaini ubora wa utendaji kazi wa watumishi hao katika utoaji wa huduma bora kwa wananchi.
Hayo yamebainishwa leo Aprili 4, 2022 na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini kutoka OR-TAMISEMI, Bi.Nteghenjwa Hosseah kupitia taarifa ya wakuu wa vitengo vya manunuzi na ugavi waliohamishwa vituo , wanaokaimu na kubakishwa kwenye vituo vya awali.
"Kutokana na tathimini hiyo na ili kuboresha utendaji kazi wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI iliwabadilishia majukumu baadhi ya wakuu wa vitengo, hivyo mnamo mwezi Machi, 2022 na kupelekea uhitaji wa wataalamu wengine wa manunuzi na ugavi kubadilishiwa vituo vya kazi na kukaimu kujaza nafasi zilizoachwa wazi na wakuu wa vitengo hivyo.
"Hata hivyo, kuna baadhi ya wakuu wa vitengo vya manunuzi na ugavi ambao wameendelea kubaki kwenye vituo vyao vya awali,"amefafanua Bi.Hosseah.
Amesema,tathimini hiyo inaendelea kwa wakuu wa idara na vitengo vilivyobakia , sambamba na watumishi wengine wote ili kubaini utendaji kazi wao katika kuwahudumia wananchi kwenye mamlaka za Serikali za mitaa.
Aidha, Bi.Hosseah amesema kuwa, tathimini hiyo itakuwa ikifanyika kila nusu mwaka na kila baada ya mwaka kukamilika.
"Uhamisho wa baadhi ywa wakuu wa Kitengo cha Manunuzi na Ugavi ni kwa mujibu wa barua ya Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ya mwaka 2006 iliyokasimu madaraka kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-TAMISEMI,"ameongeza.
Ifuatayo hapa chini ni orodha ya majina ya watumishi wa vitengo vya ununuzi na ugavi wanaohamishiwa kwenye vituo vingine, wanaokaimu;
WANAOENDELEA KUBAKIA VITUO VYAO