NA GODFREY NNKO
MAMLAKA ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imetangaza bei kikomo za bidhaa za mafuta ya petroli hapa nchini. Bei hizi zimeanza kutumika kuanzia leo Jumatano,Aprili 6, 2022.
Mkurugenzi
wa Petroli nchini,Bw.Gerald Maganga wakati akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dodoma Machi 5,2022 kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA,
Mhandisi Geoffrey Chibulunjeamesema,bei za rejareja na jumla za mafuta ya
petroli,dizeli na mafuta ya taa yaliyopokelewa kupitia Bandari ya Dar es
Salaam zimeongezeka ikilinganishwa na toleo lililopita la Machi 2,2022.
Amesema
kuwa, Aprili,2022 bei za rejareja za petroli, dizeli na mafuta ya taa
zimeongezeka kwa shilingi 321 kwa lita sawa na asilimia 21.45 mtawalia.
Maganga
amesema,toleo lililopita bei za jumla za petroli, dizeli na mafuta ya
taa zimeongezeka kwa shilingi 320.33 kwa lita sawa na asilimia 13.29,
shilingi 288.50 kwa lita sawa na asilimia 12.69 na shilingi 472.41 kwa
lita sawa na asilimia 22.72 mtawalia.Soma kwa kina hapa>>>
Zifuatazo hapa chini ndiyo bei elekezi kulingana na kila eneo hapa nchini;