Muungano wa nchi uhuru ya Tanganyika na Zanzibar uliasisiwa Aprili 26, 1964, chini ya waasisi Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Hayati Abeid Amani Karume Rais wa Kwanza wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, waliiasisi Muungano huu wa kipeekee duniani kwa kuzingatia nadharia za kiundugu na kijamaa kati ya Watanganyika na Wazanzibar, hii ni katika kuleta umoja, amani na upendo.
Muungano wetu ni nguzo pekee katika kulinda amani na umoja miongoni mwetu.ni alama ya kiupekee kama taifa.Daima tutauenzi na kuhudumisha milele na milele kwa masilahi mapana ya taifa. Uongozi wa DIRAMAKINI BLOG unawatakia Watanzania wote heri ya Miaka 58 ya Muungano.