Rais Samia ashinda Tuzo ya AfDB ya Miundombinu Afrika 2022

NA DIRAMAKINI

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amechaguliwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Africa Road Builders–Babacar Ndiaye Trophy kwa mwaka 2022.
Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, akiwa na Rais wa AfDB, Akinwumi Adesina pembeni yake, wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika barabara ya mzunguko wa nje jijini Dodoma mwezi Februari. (Picha na AfDB).

Tuzo hiyo inatolewa kwa watu mashuhuri barani Afrika ambao wameonesha dhamira yao ya kuendeleza sekta ya miundombinu ya usafiri katika bara hilo.

Kamati ya uteuzi wa tuzo hiyo imempongeza Rais Samia kwa ungozi wake na namna Serikali yake ilivyojipanga kuwezesha sekta ya miundombiu nchini Tanzania.

"Ni kwa uongozi wake binafsi, uwekezaji mkubwa na kujitolea katika kupanua barabara na mtandao wa reli nchini Tanzania. Tunatuma pongezi zetu za dhati kwa Rais Samia Suluhu Hassan na watu wa Tanzania," amesema Msemaji wa Taasisi ya ARB, George Orido.

Amesema kamati ilibaini dola milioni 290 zilizotolewa na Benki ya Maendeleo ya Afrika kusaidia ufufuaji wa usafiri wa barabara, reli na anga nchini Tanzania zilileta matokeo bora. Pia ilizingatia mkataba wa dola milioni 172.2 uliosainiwa na Kampuni ya China Corporation Limited kuipatia nchi mabehewa ya kisasa ya mizigo 1,430 ili kutekeleza mpango kabambe wa Shirika la Reli la Tanzania (TRC).

Kutokana na hali huyo pia kamati ilibaini kuanza rasmi kwa ujenzi wa mradi wa kihistoria wa ujenzi wa barabara ya mzunguko wa nje kuzunguka mji wa Dodoma, ambapo mradi huo ulizinduliwa na Rais Samia mwezi Februari 11, mwaka na kuhudhuriwa na Rais wa Benki ya Maendeleo Afrika, Dkt. Akinwumi A. Adesina.

Kwa sasa Rais Samia ni rais pekee mwanamke barani Afrika, ambapo aliingia madarakani Machi 2021, baada ya kufariki kwa mtangulizi wake, Rais John Magufuli, ambapo wakati huo yeye alikuwa Makamu wa Rais.

Kwa mwaka 2021 Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, alishinda tuzo hiyo.

Tuzo hiyo lilianzishwa kwa heshima ya Babacar Ndiaye, ambaye alikuwa Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika kutoka mwaka 1985 hadi 1995.

Aidha,tuzo hiyo kwa mwaka 2022 itatolewa katika mkutano wa mwisho wa Wajenzi wa Barabara Afrika, ambao umepangwa kufanyika pamoja na Benki ya Maendeleo ya Afrika, Mei mwaka huu jijini Accra, Ghana.

Kwa ufadhili wa Benki ya Maendeleo Afrika, chini ya Rais wa benki hiyo, Dkt. Adesina tuzo ya Wajenzi wa Barabara Afrika Babacar Ndiaye Trophy imeandaliwa na Acturoutes, Jukwaa la Habari kuhusu Miundombinu na Barabara barani Afrika, na Shirika la Media for Infrastructure and Finance in Africa (MIFA), mtandao wa wanahabari wa Afrika waliobobea katika miundombinu ya barabara.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news