NA DIRAMAKINI
RAIS
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan
amemfuta kazi Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi na Mtendaji Mkuu wa
Bohari ya Dawa (MSD).
Hatua
hiyo inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Serikali (CAG) kubaini bohari hiyo ilishikilia zaidi ya shilingi Bilioni
14 za hospitali kwa mwaka mzima bila kupeleka madawa na vifaa tiba.
Katika
taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu, Bi.
Zuhura Yunus jijini Washington DC nchini Marekani, Rais Samia amemteua
Afisa Mwandamizi katika Kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PwC), Bi.
Rosemary Slaa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bohari ya Dawa.
Pia
amemteua Kiongozi Mkuu wa Mradi wa USAID Global Health Supply Chain
Technical Assistance, Bw. Mavere Tukai kuwa Mtendaji Mkuu wa MSD.