NA DIRAMAKINI
DIMBA la Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam limetawaliwa na shangwe kila kona kutokana na kabumbu safi linalotandazwa na Simba SC dhidi ya USGN.
Katika dakika za kwanza wawili hao walionekana kutoshana nguvu, hivyo kwenda mapumziko ubao ukisoma sufuri kila upande.
Simba SC walikwama kutupia kupitia kwa Pape Sakho aliyekosa nafasi mbili, Sadio Kanoute nafasi tatu za kufunga.
Pia Kanoute kwa kucheza faulo ameonyeshwa kadi ya njano na mwingine kwa Simba ni Joash Onyango ambaye hakuwa na chaguo alimchezea faulo Adebayo Victorean.
Simba wamepiga kona 10 USGN 0 huku mashuti yakiwa 10 na moja limelenga lango.
Kipindi cha pili kilianza kwa Kanoute ndani ya dakika ya 63 kutupia bao safi ambalo lilidumu hadi dakika ya 68, Mugalu aliwanyanyua tena mashabiki wa Simba kwa bao tamu.
Bao hilo lilidumu dakika chache, kabla ya kutupa jalo safi ambalo limeiwezesha Simba SC hadi muda huu kuongoza kwa mabao matatu kwa sifuri. Huku bao la nne likitupiwa na wageni wenyewe.