"Kwa kifupi, ukiangalia madhara na madhila ya vita hivi ni pigo kubwa kwa Taifa hili na Dunia nzima, kwa hiyo inapokuja nyumbani Tanzania,ongezeko la bei ya mafuta, kama alivyosema Mheshimiwa Rais Mama Samia, si kwamba ni kwa Tanzania tu, hili ni suala la kidunia, kwa hiyo ni wakati wa Watanzania ambao tunaelewa hili jambo kwa upana, kuwaeleza wenzetu kwa lugha nyepesi na rahisi.
"Kwamba gharama za maisha zinazotokea kwa sasa, kupanda kwa vitu bei na mfumuko wa bei na kupanda bei za mafuta si suala la Serikali iliyopo madarakani, hili ni suala la Dunia na ni madhara yanayotokea kutokana na vita inayoendelea kati ya Urusi na Ukraine,kwa hiyo watanzania tuendelee kuwa wamoja, tuendelee kuchapa kazi kwa bidii, tuendelee kushirikiana na Rais wetu Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kulijenga Taifa letu,"Bw. Edwin Ndaki, diaspora nchini Finland.