Uingereza kuendelea kuunga mkono sera ya uboreshaji elimu Tanzania

NA DIRAMAKINI

SERIKALI ya Uingereza imesema inaunga mkono sera ya uboreshaji elimu kwa kuzindua mradi wa Shule Bora.

Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala ya Afrika, Amerika ya Kusini na Visiwa vya Karibiani, Vicky Ford amesema, mradi huo unahudumia watoto milioni nne kwenye mikoa tisa hapa nchini.
Akizindua mradi huo kwenye Shule ya Msingi Mkoani Halmashauri ya Mji Kibaha amesema, mradi huo unalenga kuhakikisha watoto wanakwenda shule kwa muda uliopangwa hasa wa kike ambao mara nyingi wamekuwa hawamalizi shule kutokana na changamoto mbalimbali.

Ford amesema kuwa, Serikali ya Uingereza imeamua kuwekeza kwenye sekta ya elimu ili kuwawezesha watoto kupata elimu bora.

Amesema kuwa, mradi huo wa elimu na utawajengea uwezo walimu huku watoto wote pamoja na wenye mahitaji maalumu wanakuwa shule ambapo nusu ni wa kike kuwa shuleni kubaki kwa muda unaotakiwa.

Naye Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda amesema kuwa, mradi umefadhiliwa na Uingereza kwa lengo la kuongeza ubora wa elimu na kuhakikisha wanafunzi wanaingia madarasani na kusoma ikiwemo kuboresha ufundishaji madarasani.

Mkenda amesema kuwa, pia mradi unalenga kuwawezesha walimu waweze kuboresha ufundishaji na unaendana na azma ya serikali kuboresha elimu nchini ili iwe na ubora hususani mkoani Pwani, Katavi, Kigoma, Mara,Tanga, Dodoma, Singida, Rukwa na Simiyu.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Abubakari Kunenge amesema, wanashukuru kwa kupewa mradi huo, hivyo watautunza na kuuangalia vizuri ili ulete manufaa kwa wananchi wa mkoa wa Pwani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news