*MAWINGU KIASI, MVUA NA NGURUMO ZINATARAJIWA KATIKA MAENEO MACHACHE
NA GODFREY NNKO
UTABIRI wa hali ya hewa kwa saa 24 zijazo kuanzia saa tatu usiku wa leo Aprili 5,2022 unaletwa na mchambuzi, Mohamedi Hamisi kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, Ruvuma,Kagera, Geita, Kigoma, Katavi, Rukwa, Songwe, Mbeya na Njombe inatarajiwa kuwa mvua na ngurumo kwa maeneo machache na vipindi vya jua.
Mikoa ya Lindi, Mtwara na Kusini mwa Mkoa wa Morogoro inatarajiwa mvua nyepesi kwa maeneo machache na vipindi vya jua.
Aidha, Tabora, Iringa, Visiwa vya Unguja na Pemba, Dodoma, Singida, Dar es Salaam, Tanga, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Shinyanga, Simiyu, Mara na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia) inatarajiwa kuwa na vipindi vya jua.
Wakati huo huo, upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kutoka Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya kilomita 20 kwa saa kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kusini.
Aidha, hali ya bahari kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kuna matarajio ya mawimbi madogo hadi makubwa kiasi.
WEATHER FORECAST FOR THE NEXT 24 HOURS: ISOLATED THUNDERSHOWERS ARE EXPECTED OVER FEW AREAS