*MAENEO MENGI YANATARAJIWA HALI YA UKAVU NA VIPINDI VYA JUA
NA GODFREY NNKO
UTABIRI wa hali ya hewa saa 24 zijazo kuanzia 3:00 usiku leo Aprili 8,2022 unaletwa na mchambuzi Magreth Massawe kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).
Kwa mujibu wa TMA, mikoa ya Ruvuma, Lindi na Mtwara inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Kusini mwa Mkoa wa Morogoro pamoja na Mikoa ya Songwe, Mbeya na Njombe inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
Mikoa ya Rukwa, Iringa, Dodoma, Singida, Dar es Salaam, Tanga, Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Kigoma, Katavi, Tabora, Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Kagera, Simiyu, Shinyanga, Geita, Mwanza na Mara pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
Pia upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani yote huku hali ya bahari inatarajiwa kuwa na mawimbi makubwa kiasi. Matarajio kwa siku ya Jumapili tarehe 10, Aprili, 2022 huenda kukawa na mabadiliko kidogo.
TANZANIA WEATHER FORECAST 08.04.2022:MOST AREAS ARE EXPECTED TO DRY CONDITION AND SUNNY PERIODS
Weather forecast for the next 24 hours starting 21:00 tonight 08.04.2022 presented by weather analyst Magreth Massawe:Tanzania Meteorological Authority (TMA).